Wanawake walioweka historia
Tunapoadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake, wafuatao ni wanawake 10 ambao walizikabili changamoto kadhaa na kuacha kumbukumbuku ulimwenguni.
Mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda Nobel
Mkenya huyu, Wangari Maathai (1940-2011) alikuwa mwanamazingira na mtetezi wa haki za wanawake miaka ya 1970. Kama mwasisi wa vugu vugu la Green Belt, alikabili masuala ya jangwa, ukataji wa miti, tatizo la maji na njaa katika maeneo ya mashambani. Pamoja na kuwa ilichukua muda mrefu kwa taifa lake kumkubali, mwaka 2004, alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kwa kazi yake.
Farao wa kwanza wa Kike
Baada ya kifo cha mumewe Thutmose II, Hatshepsut alichukua usukuni kwa kuwa mwanaye alikuwa mdogo. Alikuwa mmoja wa mafarao waliofanikiwa, akitawala kwa kipindi kirefu zaidi ya mwanamke yeyote katika taifa la Misri wakati huo. Aidha warithi wake walijaribu kufuta kumbukukumbu zote za utawala wake katika historia.
Shujaa Mtakatifu
Mwaka 1425, katika kipindi cha vita vya miaka mia moja vilivyokuwa vimechacha kati ya Uingereza na Ufaransa wakati ambapo binti wa miaka 13 wa mkulima, Joan, alipata maono yake ya kwanza ya watakatifu kuokoa Ufaransa na kumfanya Charles VII atawale. Joan wa Arc alikamatwa mwaka 1430, kisha akahukumiwa na kwa kuasi dini na kuteketezwa kwa makosa hayo.
Kamanda mwenye ujasiri
Catherine II alichukua mamlaka baada ya mapinduzi ambapo mumewe aliuawa na akajitangaza kiongozi mpya wa Urusi. Alionesha uongozi wake alipoleta ufalme mkubwa wa Urusi chini ya mamlaka yake na kuongoza kwenye kampeini za kushinda himaya za Poland na Cremia. Kama kiongozi wa kike aliyetawala kwa muda mrefu Urusi, alitambuliwa kuwa Catherine Mkuu.
Malkia mwenye maono
Elizabeth I alichukua usukani kwenye kiti cha utawala wa Uingereza, wakati taifa hilo lilipokuwa kwenye zogo. Alifaulu kumaliza vita kati ya Waprotestanti na Wakatoliki, hali iliyochangia Ufalme wa Uingereza wakati wa kipindi cha upeo wa ustawi wa sanaa. Utamaduni ulistawi kupitia waandishi wa tamthilia kama vile Shakespeare.
Mtetezi wa wanawake mwenye msimamo mkali
Mtetezi wa wanawake mwenye msimamo mkali Mwaka 1903, Emmeline Pankhurst (1858-1928) alianzisha kampeini za haki ya kila mtu kupiga kura Uingereza. Matendo yao ya kupinga yalijumuisha mgomo wa kula na kampeini za kuchoma. Pankhurst alikamatwa zaidi ya mara moja, lakini alifaulu kwenye azma yake ya kuruhusu wanawake walio na zaidi ya miaka 30 kupiga kura mwaka 1918. Aliaga dunia mwaka 1928
Mwanamapinduzi aliyeuawa
Wakati ambapo wanawake hawangechaguliwa mamlakani, Rosa Luxemburg alikuwa kiongozi wa vuguvugu la mapinduzi ya kijamii na kidemokrasia nchini Ujerumani. Mwasisi wa chama cha kikomunisti cha Ligi ya Spartacus, aliongoza migomo dhidi ya vita vikuu vya kwanza. Baada ya kushindwa kwa uasi wa Spartacus mwaka 1919, aliuawa na maafisa wa Ujerumani.
Mtafiti wa harakatiredio
Mtafiti wa harakatiredio Marie Curie (1867-1934) alikuwa mwanzilishi wa utafiti wa harakatiredio na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel. Alishinda tuzo ya pili ya Nobel kwa kugundua madini ya radium na polonium. Aidha alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Sorbonne, kilichoko mjini Paris.
Mwanaharakati dhidi ya Maangamizi makubwa
Anne Frank alihifhadhi shajara kutoka mwaka 1942 hadi 1944. Katika moja ya picha zilizochapishwa katika shajara yake, akiwa na umri wa miaka 13 alikuwa akitabasamu. Miezi miwili baada ya kuchukuliwa, familia yake ilienda mafichoni eneo la Prinsengracht, Amsterdam, mwezi Julai, 1942. Aliaga dunia Machi mwaka 1945.
Mwanaharakati mdogo wa haki za wasichana
Malala Youfsafzai alikuwa na umri wa miaka 11 aliporipoti kwa shirika la habari la BBC kuhusu utawala wa kigaidi wa Taliban nchini Pakistan: Wakati shule yake ya wasichana ilipofungwa, alipigania haki yake ya elimu. Mwaka 2012, aliponea jaribio la kuuliwa. Alipopata nafuu aliandika wasifu wake: "Mimi ni Malala: Msichana aliyepigania Elimu na kupigwa risasi na Wataliban."