1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake wakisaudi wakimbilia Ujerumani

20 Februari 2019

Wanawake hao wakisaudi waliokimbilia Ujerumani bado wanaishi kwa hofu kutokana na vitisho wanavyovipokea kutoka kwa familia zao zilizoko Saudia.Wanafuatiliwa nyendo zao kwa namna mbali mbali

https://p.dw.com/p/3DkMb
Doku - 9760 Die heimliche Revolution
Picha: New docs

Wanawake wakisaudi waliokimbilia Ujerumani kuomba hifadhi wanaendelea kuishi chini ya kitisho kinachotokana na familia zao. DW ilizungumza na wanawake wanne waliokuja kuomba hifadhi Ujerumani pamoja na wataalamu wa haki za binadamu ambao wanashuku kwamba ubalozi wa Saudia unahusika.

Mmejificha wapi? tunajua hampo majumbani mwenu''Ayasha anazidi kuperuzi zaidi kusoma ujumbe.''Tutawapata. Hata mkienda mwisho wa dunia,tunao watu wanaoweza kuwaafuatilia''

Ayasha amekaa akiwa miguu peku akiwa amevalia T-shirt yake na yuko jikoni mbele yake akiangalia makabrasha. Amekusanya ujumbe wote wa vitisho aliotumiwa,ameuchapisha na kuupeleka  kuutafsiri kwa lugha ya kijerumani na wataalam rasmi wa kutafsiri lugha. Ujumbe mwingine unasomeka hivi.

'' Ubalozi una watu  wanaoweza kupata taarifa zako kupitia serikali za miji''

Ujumbe huo anasema ulitumwa kupitia nambari ya Saudia. Na ujumbe huo unatoka kwa familia yake mwenyewe. Ayasha ana umri wa miaka ya thelathini na kitu,anaishi kama mkimbizi nchini Ujerumani. Aliikimbia familia yake na mfumo wa nchi yake ambao unawaangalia hata wanawake watu wazima kama watoto na wasioweza kuyaongoza masiaha yao. Wanawake wakisaudi wanabidi kuomba ridhaa za waume zao au wazazi wao kwa takriban kila kitu wanachotaka kufanya.

Symbolbild Saudi Arabien Video zu sexueller Belästigung von Frauen
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Sarbakhshian

Hali ilikuwa sio tafauti kwa Ayasha pia alipokuwa akiishi Saudi Arabia. Kokote alikokwenda alikuwa akiandamana na mmoja wa kakazake au alikuwa akipelekwa na dereva na kurudishwa alipomaliza shughuli zake. Halafu familia yake ikalazimisha aolewe na mtu ambae hakuwahi kumuona kwa macho,ambaye alikuwa hana upendo kwake kutokea siku ya mwanzo kabisa walipozungumza.

Ayasha alianza kupanga mikakati ya kutoroka. Anakumbuka jinsi alivyoiba simu ya baba yake kisha akamzidi maarifa katika mbinu zake mwenyewe. Babake alikuwa na app inayoitwa Absher ambayo inatumika kufuatilia na kudhibiti nyendo za mtu. Abshaer ambayo ni bure inapatikana katika app store za simu zote za Android na Apple na ilianzishwa mwaka 2015 na serikali ya Saudi Arabia na inafanyiwa matangazo na wizara ya mambo ya ndani ya Saudi.

Zaidi ya watumiaji milioni 11 tayari wanaprogrammu hiyo kwa mujibu wa ukurasa wa app hiyo. App hii inatoa fursa kwa wanaume kusajili majina na nambari za hati za usafiri za wanawake wa familia zao na kisha unaweka angalizo kwamba watu hao wasiruhusiwe kusafiri kama wanavyotaka. Kwa Ayasha lakini hiyo app ya Absher badala ya kuwa mwiba kwake ilikuwa nusra na bahati:Alifanikiwa kuibadilisha nambari ya siri ya babake na kuomba mpya. Halafu akajiwekea ruhusa ya kusafiri na mwezi Agosti mwaka 2017 alipanda ndege na kuelekea Ujerumani. anasema'' sikuwa na chochote cha kupoteza''

Mwandishi: Felden,Esther/Saumu Mwasimba

Mhariri: Sekione Kitojo

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW