Wanawake wengi Uingereza wasiokuwa na mahusiano na wanaume wanakimbilia Denmark kwenda kupandikizwa mbegu za uzazi za wanaume waliojitolea mbegu zao katika maabara. Sababu inaelezwa inatokana na kukosekana wanaume wa kujitolea kutowa mbegu Uingereza tangu ilipoanzishwa sheria inayompa haki mtoto atakaezaliwa kwa njia hizo kumtafuta babake akifikia umri wa miaka 18.