1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake Sudan wakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia

26 Novemba 2024

Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Tom Fletcher ameelezea wasiwasi kuhusu kile alichokitaja kama "janga la unyanyasaji wa kingono" dhidi ya wanawake nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4nQoY
Sudan I Wanawake
Wanawake wa Sudan ambao ni wakimbiziPicha: Florian Gaertner/IMAGO

Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Tom Fletcher ameelezea wasiwasi kuhusu kile alichokitaja kama "janga la unyanyasaji wa kingono" dhidi ya wanawake nchini Sudan.

Akizungumza katika ziara yake ya kwanza katika mji wa Port Sudan, Fletcher, ambaye anaongoza Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kiutu (OCHA), amesema anahisi aibu kwamba hawakuweza kuwalinda wanawake, na anahisi aibu kwa kinachofanywa na wanaume wenzake.

Wakati wa ziara yake, Fletcher amekutana na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kujadili juhudi za "kuongeza uwasilishaji wa misaada katika mipaka na maeneo ya migogoro".Zaidi ya Wanawake na Wasichana 200 wabakwa Sudan Kusini

Mwezi uliopita ujumbe huru wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, ulirekodi kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na "ubakaji, unyanyasaji wa kingono na utekaji nyara kwa madhumuni ya kingono pamoja na madai ya kulazimishwa ndoa na biashara haramu ya binadamu".