Ujerumani imeonekana kuwa nchi yenye sehemu nzuri ya kuishi na kufanya kazi duniani. Ni mojawapo ya nchi za ulaya zinazoendelea kuwa kivutio zaidi kwa wahamiaji au wakimbizi. Sura ya Ujerumani wiki hii inamulika namna wahamiaji na wakimbizi wanawake wa kiislamu wanavyoshughulikiwa ili kukabiliana na mazingira yao mapya katika mji wa Cologne, magharibi ya Ujerumani. Muandaaji ni Fathiya Omar.