Wanawake Pakistan wavunja miiko ya mahusiano kwenye Tinder
11 Agosti 2020Faiqa ni mjasiriamali mwenye umri wa miaka 32 mjini Islamabad, na kama ilivyo kwa wanawake wengi wasio na wapenzi duniani, anatumia app za kutfuta wapenzi kuwasiliana na wanaume.
Ingawa mahusiano ya kawaida kwa wanawake ni jambo linaloendelea kuchukiza katika jamii ya kihafidhina na inayoongozw ana mfumo dume, fikira zinaanya kubadilika katika maeneo ya mijini nchini humo.
Fariqa amekuwa akitumia app ya kutafuta wachumba ya Tinder kwa miaka miwili sasa, na alisema inagawa uzoefu wake umemuweka "huru", wanaume wengi wa Pakistan hawajazoea dhana ya wanawake kujiamulia mambo yao ya kimapenzi. Wanawake wa Pakistan wanatarajiwa kulinda heshima ya familia.
"Nimekutana na baadhi ya wanaume kwenye Tinder wanaojielezea kama wenye fikira za wazi kuhusu masuala ya wanawake lakini bado wananiuliza: Kwa nini msichana mwenye heshima na msomi kama wewe unapenda kutafuta mpenzi kupitia app?" Faiqa aliiambia DW.
Utafutaji wachumba mtandoni waongezeka Asia Kusini
India inaongoza soko la app za kukutanisha wapenzi, na Pakistan inafuata nyuma kwa taratibu. Utafiti uliofanywa na Jarida la utafiti wa mawasiliano nchini Indonesia uligundua kwamba watumiaji wengi wa app ya Tinder nchini Pakistan wanatokea miji mikubwa ikiwemo Islamabad, Lahore na Karachi na kawaida wako kati ya umri wa miaka 18 na 40.
App nyingine za kukutanisha wapenzi zinazidi pia umaarufu. App ya MuzMatch inashughulikia hasa Waislamu wanaotafuta wachumba. App ya Bumble, licha ya kuwa mpya kwenye soko la utafutaji wapenzi mtandaoni, inapendelewa zaidi na wanaharakati wa wanawake nchini Pakistan, kwa kuwa wanawake ndiyo huanzisha mazungumzo.
"Kuna wanaume wachache kwenye app ya Bumble, hivyo ni salama kwa sasa kuitumia. Tinder ni maarufu sana na mtu unaemfahamu anaweza kukuona, na hivyo kukukosesha amani," alisema NImra, mwanafunzi kutoka Lahore.
Hata hivyo, wanawake wengi vijana nchini Pakistan wantumia app kwa sababu zinafanya ukutanishaji wapenzi kuwa wa faragha zaidi.
"Kwa app ya ukutanishaji, mwanamke anaweza kuchagua anchokitaka. Ni vugumu kwa wanawake kufanya hivikwa uwazi katika utamaduni wetu, sababu kwa nini app za kukutanisha wapenzi zinawapa fursa ambazo hawawezi kupata kwingineko," alisema Nabiha Meher Shikh, mwanaharakati wa kike kutoka Lahore.
Utafutaji wa ujinsia katika jamii ya kihafidhina
Sophia, mtafiti wa umri wa miaka 26 kutoka Lahore, aliiambia DW kuwa anatumia Tinder kutafuta ujinsia wake pasipo na vikwazo." !Sijali iwapo watu wananihukumu. Jamii mara zote itakuhukumu, hivyo kwa nini ujisumbue kujaribu kuwafurahisha?" alihoji.
Hata hivyo, siyo wanwake wote wanaotumia Tinder wazo wazi kama Sophia. Wasifu nyingi za wanawake wa Pakistan kwenye Tinder haziweki wazi kikamilifu utambulisho wao, huku picha zikionyesha sura zilizochongwa, mikono, au miguu, sura zilizofunikwa na nywele au kucha zilizopakwa rangi tu.
"Ikwia tutaweka majina yetu halisi au picha, wanaume wengi wana kawaida ya kutuchombeza. Iwapo hatutajibu, wanatutafuta kwenye mitandao ya kijamii na kututumia ujumbe wa ajabuajabu," alisema Alishba mwenye umri wa miaka 25 kutoka Lahore.
Aligusia pia undumila kuwili, akieleza kwamba wanaume walioko kwenye ndoa mra nyingi hutumia "ndoa zao zilizovunjika" kama kisingizio cha kuchumia wanawake wengine mtandaoni.
Kuanzishwa kwa app za kukutanisha wapenzi nchini Pakistan kumetoa pingamizi kwa miiko na kuibua mjadala kuhusu ujinsia wa wanawake, maridhiano na ngono salama.
Kwa baadhi, kuongezeka kwa umaarufu wa app za kukutanish kunafichua ukubwa wa udhibiti wa serikali juu ya miili ya wanawake na chaguo binafsi za watu.
Katibu Mkuu Ameer ul Azeem wa chama cha Kiislamu cha Jamaat-el-Islami aliiambia DW kwamba "wasichana na wavulana wanaotumia app hizi wanakutana kwa siri kwa sababu wanatambua pia kwamba hilo ni kosa.!