Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo, viongozi hao wamesema hilo ni tukio la kwanza katika historia ya Tanzania, tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Rais Samia amepongezwa kwa hatua hiyo ya kuruhusu mikutano ya hadhara iliyozuiwa mwaka 2016 na hayati Rais John Magufuli aliyetumia hoja kwamba wananchi walihitaji muda wa kufanya kazi na hivyo vyama vilipaswa kusubiri hadi wakati wa uchaguzi wa 2020.
Kwa upande wake, Kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini, alipongeza hatua ya Rais Samia, lakini akatoa angalizo kuwa, huenda wapo aliowaita wahafidhina ambao hawajapendezwa na maamuzi ya Rais:
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamemsifu Rais Samia kwa kuwarudisha Chadema katika ushiriki wa matukio ya kisiasa, yanayoandaliwa na serikali, hatua waliyoeleza kuwa ni ukomavu wa kisiasa.
Hata hivyo, mkutano huu wa waandishi wa habari na vyama vya siasa haukuhudhuriwa na chama hicho kikuu cha upinzani, CHADEMA: