Wanariadha wa Kenya wanaopeperusha bendera za nchi nyengine Olimpiki
Mwenge wa Olimpiki katika sherehe ya ufunguzi wa Rio mwaka 2016. Sio wanariadha wote katika michezo hiyo hudumisha uzalendo katika nchi zao. Hawa ni baadhi ya wanariadha mashuhuri waliobadili uraia wao.
Walio chini ya bendera ya Uturuki
Zaidi ya wanariadha wa zamani 30 wanawakilisha nchi za nje badala ya nchi zao za kuzaliwa katika mashindano ya Olimpiki ya Rio. Wanariadha hao wanajumuisha mshindi wa nishani ya dhahabu wa bara Ulaya, Polat Kemboi Arikan (kushoto) na nishani ya dhahabu Ali Kaya (kulia) watakaoiwakilisha Uturuki katika mbio za mita 10,000 za wanaume.
Raia wa Uturuki tangu mwaka 2011
Mzaliwa wa Kenya, Tarik Langat Akdag, (Patrick Kipkirui) anaiwakilisha Uturuki katika mbio za mita 3,000 kuruka viuzi. Alijipatia uraia wa Uturuki mwaka wa 2011. Tarik Langat alishinda medali ya fedha tangu mwaka 2012 na alishiriki katika mbio za kuruka viunzi na maji za mita 3,000. Hii ni kulingana na tovuti ya michezo ya wanariadha barani Ulaya.
Olimpiki ya Wakenya na Marekani
Michezo ya Olimpiki ya Rio itakuwa mara ya tano kwa Bernard Langat mwenye miaka 41 kushiriki katika mbio za mita 5,000, mbili kwa Kenya katika michezo ya Olimpiki ya Sydney mwaka 2000 na Athens mwaka 2004, na tatu kwa Marekani katika michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008, London 2012 na hii ya Rio 2016.
Alijiunga na jeshi na sasa anaiwakilisha Marekani katika michezo ya Olimpiki ya Rio
Paul Chelimo (kulia) anayeonekana na Bernard Lagat, anatokea Iten, Kenya. Ameliambia shirika la habari la AP kuwa alijiunga na jeshi la Marekani, akajipatia uraia na pia mafunzo kupitia mpango wa wanariadha jeshini. Paul Chelimo atashindana katika mbio za mita 5,000.
Mita 800 kwa Bahrain
Abraham Kipchirchir Rotich (katikati) mwenye umri wa miaka 22 anaiwakilisha Bahrain katika mbio za wanaume za mita 800. Anaonekana akiwa na Mark English pamoja na Mostafa Smaili katika mkutano wa wanaridha mwezi Julai.
Mita 3,000 kwa Bahrain
Mzaliwa wa Kenya, Ruth Jebet, anaiwakilisha Bahrain katika mbio za wanawake mita 3,000 kuruka viunzi na maji na anasemekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda, kama inavyoripoti tovuti ya gazeti la Kenya la Star. Alishinda medani ya dhahabu katika mashindano ya ubingwa wa bara la Asia 2013, na Mashindano ya Ubingwa ya Vijana ya Dunia 2014 yaliyofanyika Eugene, Oregon nchini Marekani.
Mbio za Marathon za kukumbukwa
Mwanaridha aliye na asili ya Kenya, Lucia Kimani-Marceti,c anakimbia mbio za Marathon za wanawake. Ni mwanariadha wa kwanza wa Bosnia kuwahi kumaliza michezo mitatu ya Olimpiki. Mwaka 2004 alikuwa mkimbiaji asiye maarufu sana kushiriki katika mbio za Marathon za Salzburg. Katika michezo hiyo alikutana na mumewe mwanariadha Sinisa Marcetic.