1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wananchi wa Nigeria leo kuwachagua wabunge

2 Aprili 2011

Wanigeria leo wanapiga kura kuchagua bunge jipya katika mfululizo wa chaguzi zitakazofanyika hadi Aprili 16.

https://p.dw.com/p/10mHM
Wananchi wa Nigeria wakipiga kuraPicha: DW

Uchaguzi huu mkuu ni jaribio la kuona iwapo nchi hiyo yenye watu wengi kabisa barani Afrika inaweza kuachana na historia ya uchaguzi wenye udanganyifu na vurugu.

Tume ya Uchaguzi ina matumaini kuwa daftari jipya la wapiga kura, taratibu imara za kupiga kura na usalama bora zitasaidia kukomesha udanganyifu, lakini tayari kulikuwa na ghasia katika mikoa kadhaa wakati wa kipindi cha kampeni.

Nigeria Ibrahim Shekarau und Nuhu Ribadu
Baadhi ya wagombea wa urais Nigeria, Ibrahim Shekarau, (shoto) na Nuhu RibaduPicha: AP

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Nigeria, Attahiru Jega amesema kuwa miaka 12 iliyopita, nchi hiyo ilirejea katika utawala wa kidemokrasia na ilianza safari ambayo wengi walitarajia sasa itakuwa imeleta mfumo thabiti wa kidemokrasia lakini yasikitisha kuwa bado haijafikia hali hiyo.

Mipaka ya nchi hiyo ilifungwa kabla ya uchaguzi huo kuanza hii leo na maafisa wa uchaguzi, vikosi vya usalama na wafanyakazi wa dharura pekee ndio wanaoruhusiwa kusafiri katika barabara wakati wa saa za kupiga kura.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE)
Mhariri: Prema Martin