Wanamgambo wakabiliwa na maisha magumu DRC
24 Januari 2022Matangazo
Ripoti ya shirika la habari la AFP ikiwanukuu baadhi ya wanamgambo hao imesema mwanzoni mwa mwezi huu wanamgambo hao waliandamana kupinga hali ngumu ya maisha katika kambi ya Mubambiro.
Kiongozi wa wanamgambo hao wa zamani wa kundi la wahutu´la Nyatura, Tumaini Bivundi amesema baada ya kuweka chini silaha kwa ajili ya kuunga mkono amani walitarajia kuangaliwa vizuri.
soma zaidi: Wanamgambo wa CODECO wakubali kustisha vita DRC
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya AFP wanamgambo wengi waliojisalimisha na kuanza maisha ya kiraia wanakabiliwa na hali ngumu na wengi wanakufa kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji yasiyo salama.
Mpaka sasa wanamgambo 13 wa zamani wamekufa.