SiasaSudan
Wanamgambo wa RSF waonesha dhamira ya kusitisha mapigano
3 Januari 2024Matangazo
RSF imetia pia saini tamko na muungano wa kiraia "Taqadum" na kulitaka pia jeshi kufanya hivyo.
Vita vya miezi tisa nchini Sudan, ambayo sasa inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi duniani wa watu walioyahama makazi yao, umeharibu miundombinu ya nchi hiyo na kuzusha tahadhari za kutokea baa la njaa.
Majaribio ya kumaliza mzozo huo kwa njia ya mazungumzo yakiongozwa na Marekani na Saudi Arabia, hadi sasa yameambulia patupu huku makubaliano ya awali ya kuwalinda raia yakipuuzwa.
Kwa kutia saini kile kinachoitwa "Azimio la Addis Ababa" ambalo linakusudiwa kutumika kama msingi wa kufanyika mazungumzo zaidi na suluhisho la kisiasa, RSF imeonyesha nia ya wazi ya kuvimaliza vita hivyo.