1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wawili wa Mali wauawa

Josephat Charo
14 Februari 2022

Wanajeshi wawili wa Mali wameuwawa kaskazini mwa nchi hiyo katika shambulizi dhidi ya kituo chao linalodaiwa kufanywa na wapiganaji wa jihad.

https://p.dw.com/p/46ysC
Mali | Operation Barkhane
Picha: Benoit Tessier/REUTERS

Jeshi la Mali limeripoti katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la kigaidi lililojihami na silaha lilikishambulia kituo cha jeshi cha Niafunke Jumapili alfajiri ambapo wanajeshi hao waliuliwa.

Jeshi aidha limesema wapiganaji watano waliuwawa.

Vifo hivyo ni vya kwanza kuripotiwa na jeshi la Mali tangu ripoti ya Januari tano ya vifo sita wakati wa makabiliano mnamo mwezi Novemba na Desemba.

Wakati huo huo, jeshi la Mali limedai kuhusika na vifo vya wapiganaji kadhaa wa jihadi na uharibifu wa kambi zao tangu kuanza kwa operesheni Keletigui mwezi Desemba mwaka uliopita.

Mali imekuwa ikipambana kudhibiti uasi wa wapiganaji uliozuka mnamo 2012 ambao umeenea katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger.