1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi watatu wa Ethiopia wauliwa Mogadischu

Oumilkher Hamidou4 Januari 2009

Bomu laripuka barabarani wakati wanajeshi wa Ethiopia wasafisha njia kuweza kurejea nyumbani

https://p.dw.com/p/GRp0

Mogadischu:


Wanajeshi wanne wa kiethiopia wameuwawa baada ya bomu kuripuka barabarani leo asubuhi mjini Mogadischu nchini Somalia.Bomu hilo limeripuliwa karibu na kituo cha ukaguzi cha vikosi vya ulinzi vya Somalia,katika njia inayounganisha mji mkuu na sehemu ya magharibi ya nchi hiyo.Wanajeshi wa Ethiopia walikua katika opereshini ya kusaka miripuko iliyofichwa katika sehemu hiyo,kwa lengo la kutakasa njia kwaajili ya malori yanayosafirisha wanajeshi na vifaa vyao."Ni miripuko mkubwa kabisa kuwahi kusikika katika eneo hilo" amesema hayo mkaazi mmoja wa mtaa wa Shamso Muhidin.Vikosi vya Ethiopia vilivyoingilia kati mwaka 2006 kuwatimua wafuasi wa mahakama za kiislam nchini Somalia, vimeanza kuihama nchi hiyo inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 1991.