Wanajeshi wajaribu kuasi Mali, milio ya risasi nje ya kambi
18 Agosti 2020Afisa moja katika kituo hicho cha jeshi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba milio hiyo ya risasi ilikuwa kitendo cha uasi na kwamba wanajeshi wengi hawafurahishwi na hali ya kisiasa, na kuongeza kuwa wanataka mabadiliko.
Tukio hilo limetokea wakati sawa ambapo upinzani unapanga kurudia maandamano dhidi ya rais wa taifa hilo maskini, Ibrahim Boubacar Keita. Daktari moja mjini Kati, ameiambia AFP kuwa kulikuwepo na wanajeshi wengi na walikuwa na wasiwasi.
Soma pia Keita aunda serikali mpya kukabili mkwamo wa kisiasa Mali
Ubalozi wa Ufaransa, ambayo ndiyo mkoloni wa zamani wa Mali, umependekeza kupitia mitandao ya kijamii, kwamba kila mtu abakie nyumbani.
Lakini afisa mmoja katika wizara ya mambo ya ulinzi ya Mali, amesema hakuna uasi wowote ulikuwa unaendelea, na kuongeza hata hivyo, kwamba serikali inafuatilia hali hiyo kwa karibu.
Mwanadiplomasia wa Magharibi mjini Bamako, ambaye alikataa kutajwa jina, aliyaelezea matukio hayo kama jarbio la usasi.
Soma pia Jumuiya ya ECOWAS na juhudi za kidiplomasia nchini Mali
Mali amekuwa katika mzozo mkubwa wa kisiasa tangu mwezi Juni, wakati ambapo rais Keita akikabiliwa na vuguvugu la maandamano linalomtaka ajiuzulu.
Maandamano ya vuguvugu la Juni 5
Vuguvugu hilo lililopewa jina la Juni 5, kutokana na tarehe ya maandamano yake ya kwanza, limekuwa likielezea hasira kuhusiana na hali mbaya ya kiuchumi, rushwa iliyokithiri serikalini na mzozo wa wapiganaji wa itikadi kali unaogharimu maisha ya watu.
Soma pia Waziri Mkuu wa Mali akataa kujiuzulu
Kampeni ya vuguvugu hilo dhidi ya Keita iligeuka mzozo mwezi uliopita, baada ya watu 11 kuuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama, katika muda wa siku tatu za machafuko kufuatia maandamano hayo.
Tangu wakati huo, kundi hilo limakataa juhudi za upatanishi na rais Keita mwenye umri wa miaka 75, na limeapa kuendelea na maandamano dhidi yake.
Siku ya Jumatatu, lilitangaza kwamba lingeitisha maandamano ya kila siku ambayo yangehitimishwa kwa mkutano mkubwa siku ya Ijumaa.
Unaweza kusoma pia Juhudi za kutafuta upatanishi Mali zagongwa mwamba
Maandamano yalitarajiwa kuanza Jumanne, kwa msafara wa kujenga ufahamu wa maelfu ya magari yakizunguka mji, ingawa haikubainika wazi iwapo hili lilikuwa linaendelea kama ilivyopangwa.
Upinzani mara kwa mara umetupilia mbali mapendekezo ya kumaliza mzozo wa Mali yaliowasilishwa na wapatanishi wa kimataifa na badala yake kutoa madai ya kumtaka Keita ajiuzulu.
Soma zaidi Imam Dicko haoni haja ya Rais Keita wa Mali kujiuzulu
Washirika na majirani za Mali wanahaha kuepusha nchi hiyo kutumbukia tena katika machafuko.
Maeneo makubwa ya nchi hiyo tayari yako nje ya udhibiti wa serikali, ambayo inapambana kudhibiti uasi wa wanamgambo wa Kiislamu, uliozuka kwa mara ya kwanza mwaka 2012 na umegharimu maisha ya maelf ya raia.
Kushinda kumalizwa kwa mzozo huo kumechangia kuchochea hasira dhidi ya utawala wa Keita nchini Mali.
Vyanzo: afpe, rtre