SiasaUrusi
Wanajeshi wa Urusi waimarisha operesheni yao Bakhmut
28 Februari 2023Matangazo
Rais Volodymyr Zelenskiy pia alisema jana usiku kwamba adui yao anaharibu kila kitu kinachoweza kutumiwa kulinda ngome zao. Wakati huo huo, Rais wa Urusi Vladmir Putin ameiagiza idara ya usalama ya FSB kuimarisha usalama katika majimbo manne yanayodhitibiwa kwa sehemu na askari wake na pia kupambana na kile alichokielezea kuwa ni ongezeko la operesheni za kijasusi na hujuma dhidi ya Urusi zinazofanywa na Ukraine na nchi za Magharibi.
Aliyasema hayo baada ya gavana mmoja wa kikanda kusema ndege isiyoruka na rubani ilianguka karibu na kituo cha kusambaza gesi asilia katika kile kinachodaiwa kuwa shambulizi lililoshindikana karibu na mji wa Kolomna, kusini mashariki mwa Moscow.