Wanajeshi wa Ujerumani wawasili Lithuania
9 Aprili 2024Hii ni mara ya kwanza tangu Vita vya Pili vya Dunia kwa wanajeshi wa Ujerumani kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya kukaa muda mrefu.
Wanajeshi wapatao 24 waliwasili nchini Lithuania siku ya Jumatatu (Aprili 8), wakiwatangulia wenzao 150 ambao watajiunga nao baadaye mwaka huu.
Soma zaidi:Wanajeshi wa Ujerumani wawasili Lithuania, kwa mara ya kwanza tangu Vita vya Pili vya Dunia
Idadi kamili ya wanajeshi wa Ujerumani watakaopelekwa nchini humo itakuwa 5,000 kufikia mwishoni mwa mwaka 2027.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, aliwaaga wanajeshi hao mjini Berlin, akisema ilikuwa ni "siku muhimu" kwa jeshi la nchi yake, Bundeswehr.
Mjini Vilnius, Waziri wa Ulinzi Laurynas Kasciunas, aliwapokea wanajeshi hao akisema ni mfano mzuri kwa mataifa yote wanachama wa NATO upande wa mashariki mwa Ulaya, yanayopakana na Urusi na mshirika wake, Belarus.