1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ujerumani wajeruhiwa Afghanistan.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVpW

Kabul.

Wanajeshi watatu wa Ujerumani wamejeruhiwa katika shambulio dhidi ya msafara wao kaskazini mwa Afghanistan. Jeshi la Ujerumani limeripoti kuwa wanajeshi wawili wamejeruhiwa vibaya na watatu amepata majeraha madogo wakati gari yao ilipopinduka baada ya kulipuliwa na bomu kando ya barabara karibu na mji wa Kunduz mapema leo Alhamis.

Waliojeruhiwa watarejeshwa Ujerumani kwa ajili ya matibabu. Jana mwanajeshi mmoja wa Denmark aliuwawa na mwingine kujeruhiwa katika mapambano ya silaha dhidi ya wapiganaji wa Taleban kusini mwa Afghanistan.