1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani wajizatiti zaidi Haiti.

6 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFfd

PORT-AU-PRINCE: Nchini Haiti wanajeshi wa Kimarekani wamezidi kuingia miji mbali mbali kwa shabaha ya kuhakikisha usalama. Pamoja na Mji mkuu, sasa wameingia pia miji ya Cap Haitian Na Gonaives. Iko mipango ya kupelekwa wanajeshi wengine wa Kimarekani katika miji mengine ya Haiti. Katika mji mkuu Port-au-Prince wafuasi zaidi ya 4000 wa Rais Jean-Bertrand Aristide aliyekimbilia Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamefanya maandamano ya kupinga utanuzi huo wa wanajeshi ya Kimarekani nchini Haiti. Jamhuri ya Afrika ya Kati imemwita Aristide aache kutoa matangazo ya hadharani. Rais huyo wa zamani wa Haiti aliwahi kujiita mahabusi wa kisiasa na kuishutumu Marekani kumlazimisha kuihama nchi yake.