1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ethiopia wawarudisha nyuma wapiganaji wa Amhara

9 Agosti 2023

Askari wa Ethiopia wamewarudisha nyuma wapiganaji katika miji miwili ya eneo lenye machafuko la Amhara. Haya ni kwa mujibu wa wakaazi, baada ya maafisa wa eneo hilo kuripoti kuwa amani imerejeshwa kwa kiasi fulani.

https://p.dw.com/p/4Uy0a
Äthiopien Soldaten feiern Sieg
Picha: Alexander Joe/AFP/dpa/picture-alliance

Hakujawa na idadi rasmi ya vifo kutokana na machafuko ya Amhara, lakini madaktari wawili wameliambia shirika la habari la AFP kuwa raia kadhaa wameuawa na wengi kujeruhiwa.

Shirika la WFP larejesha msaada wa chakula Ethiopia

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed wiki iliyopita ilitangaza hali ya hatari ya miezi sita katika mkoa huo baada ya ghasia kuzuka kati ya wapiganaji wa eneo hilo na wanajeshi wa serikali kuu.

Machafuko hayo mapya katika nchi hiyo ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika yanajiri miezi tisa tu baada ya kumalizika kwa vita vikali vilivyodumu kwa miaka miwili katika mkoa jirani wa Tigray ambavyo pia viliwahusisha wapiganaji wa Amhara.