1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Wanajeshi 14 wa Somalia wauawa katika shambulizi la bomu

21 Oktoba 2023

Takriban wanajeshi 14 wa Somalia wameuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika kambi moja ya jeshi karibu na mji mkuu Mogadishu

https://p.dw.com/p/4Xr6H
Wanajeshi wa Somalia wahudhuria hafla ya kufuzu baada ya mafunzo kutoka jeshi la uturuki mjini Mogadishu mnamo Desemba 23, 2017
Wanajeshi wa Somalia wahudhuria hafla ya kufuzu baada ya mafunzoPicha: Sadak Mohamed/AA/picture alliance

Afisa mmoja wa polisi Mohamed Dahir, ameliambia shirika la habari la dpa kwamba wamepoteza wanajeshi 14 katika shambulio hilo la kigaidi . Dahir ameongeza kuwa raia wawili pia waliuawa huku milipuko hiyo ikiharibu nyumba nyingi karibu na kambi hiyo.

Dahir amesema kuwa mshambuliaji huyo alilenga kambi hiyo iliyo umbali wa kilomita 15 Kusini Magharibi mwa Mogadishu kwasababu inamilikiwa na polisi wa jeshi la Somalia, kikosi kipya cha wataalamu kinacholenga kuimarisha usalama katika mji huo mkuu na maeneo yanaouzunguka.

Maafisa wa idara ya ujasusi pia wamuawa katika shambulio hilo

Afisa mmoja wa usalama Abdimalik Hussein, ameliambia shirika la habari la dpa kwamba maafisa wa idara ya ujasusi na usalama wa kitaifa ni miongoni mwa wale waliouawa katika shambulio hilo.

Kupitia redio yake ya Andalus, kundi linalojiita dola la kiislamu IS, limedai kuhusika katika shambulio hilo lakini limesema limewauawa takriban wanajeshi 50.