1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 11 wa Burundi wauawa Somalia

Aboubakary Jumaa Liongo/AFP23 Februari 2009

Wanajeshi 11 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika, nchini Somalia wameuawa kufuatia shambulizi la maroketi kwenye kambi yao lililofanywa na wanamgambo wa kislam.

https://p.dw.com/p/GzOd
Wanamgambo wa kundi la Al-ShababPicha: AP

Msemaji wa Umoja wa Afrika El Ghassim amesema kuwa wanajeshi hao waliyouawa wanatoka Burundi, ambapo kambi yao ilipigwa na maroketi, lakini kundi la wanamgabo wa kiislam la Al Shabaab limesema kuwa mauaji hayo yalitokana na mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga waliyoyafanya.


Kundi hilo la Al Shabaab ambalo ni kati ya makundi yaliyokuwa yakiendesha mapambano dhidi ya majeshi ya Ethiopia hivi sasa linadai kuondoka kwa majeshi yote ya kigeni nchini humo.


Vikosi vya kulinda amani vya Umoja huo wa Afrika huko nchini Somalia, vinaundwa na wanajeshi kutoka Uganda na Burundi pekee.