Serikali ya Uganda imethibitisha kuwa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikimbilia nchini humo mwishoni mwa wiki kufuatia mapigano makali na wapiganaji wa M23 eneo la Bunagana. Aidha imefahamika kuwa mji huo wa Bunagana upande wa DRC uko mikononi mwa wapiganaji hao. Kutoka Kampala mwandishi wetu Lubega Emmanuel alitutumia taarifa ifuatayo.