Wanaharakati wataka walemavu walindwe dhidi ya joto kali
26 Juni 2023Matangazo
Shirika hilo limesema watu wenye ulemavu nchini Uhispania na katika nchi nyingine za Ulaya wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa sana kutokana na hali ya joto na jua kali katika kipindi cha kiangazi.
Katika ripoti yake, shirika hilo limesema walemavu wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha, kuumizwa kimwili, kisaikolojia na matatizo ya afya ya kiakili kutokana na joto kali na hasa wanapoachwa kujishughulikia wenyewe wakati kukiwa na hali hatari ya viwango vikubwa vya joto.
Jonas Bull, mtafiti msaidizi katika shirika la Human Rights Watch amesema hali ya kushindwa kufikika maeneo mbali mbali katika maeneo ya mijini imechangia kuongeza matatizo kwa walemavu.