1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Wanaharakati Wataka haki za kijamii, kiuchumi kwa raia

31 Agosti 2023

Wanaharakati wa haki za kijamii na kiuchumi barani Afrika wanataka Umoja wa Afrika uilazimu mataifa ya bara hilo kuwekeza zaidi ipasavyo katika utoaji huduma za jamii ikiwemo afya, elimu na miundombinu.

https://p.dw.com/p/4VngP
Äthiopien 60. Jahrestag der Afrikanische Union (AU)
Picha: Solomon Muchie/DW

Wanaelezea kuwa utegemezi wa mataifa hayo kwa ufadhili wa kigeni kugharamia huduma hizo nyeti za kijamii ni kinaya pale zinapotumia kodi wa raia kwa maslahi ya viongozi kujiimarisha katika utawala.

Kulingana na wadau, wakati umewadia kwa raia wa Afrika kudai haki zao kuhusiana na huduma za afya,elimu na miundombinu kutoka kwa serikali zao bila kuhamasishwa na mataifa wala asasi za kigeni.

Wanaamini kuwa Umoja wa Afrika ni chombo muhimu katika kushinikiza mataifa kufanya hivyo ukiwafanya wote kutelekeza mikataba na itifaki mbalimbali zilizopitishwa hapo awali kuhusiana na uwekezaji stahiki katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

Soma pia:Wakuu wa nchi Afrika wakutana Tanzania

Kwa mfano kwa mujibu wa mkataba wa Abuja, mataifa yanatakiwa kuwekeza asilimia 15 ya bajeti zao katika sekta ya afya.

Lakini kwa wastani mataifa yanawekeza chini ya asili mia saba na kuyaachia mataifa ya kigeni kuziba pengo kubwa katika kugharimia huduma hizo.

Vivyo hivyo katika sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa bara hilo, uwekezaji ni mdogo. 

Südafrika Sport l Rugby, Training in einer Grundschule in Soweto
Watoto kutoka Afrika Kusini wakicheza mpra wa mikonoPicha: Jerome Delay/AP/picture-alliance

Wakati huo huo, wadau wanazitaka serikali kuondokana na mienendo ya kutoa kandarasi kwa sekta binafsi kuendesha huduma za elimu na afya au kuacha watu binafsi kudhubiti huduma hizo kama biashara kwao.

Hii kwa mtazamo wao huchangia katika ufisadi na pia utoaji duni wa huduma hizo.

Angella Kasule Nabwowe ni mkurugenzi wa ISER ambalo ni shirikisho linalohamasisha kuhusu haki za kijamii na kiuchumi barani Afrika.

"Msichukue haki yetu na kuwapa watu wengine kwa kuwanufaisha." Alisema.

Raia wasiwategemee viongozi katika misaada

Wadau hao wanahimiza raia wa Afrika wafahamu kuwa pale wanapowachagua viongozi wasiwategemee kutoa misaada ya moja kwa moja kwao.

Ila wafahamu kuwa wao ni wawakilishi wao katika kuhakikisha kuwa raslimali za taifa zinagawanywa na kutumiwa kwa usawa moingoni mwa raia.

Huduma ya Bima ya Afya kwa wote

Hiki ndicho chanzo cha baadhi ya viongozi kuangazia kujitajirisha badala ya kuzingatia kutekeleza sera zinazowawezesha raia wao kupata huduma stahiki za umma.

Soma pia:UNDP: Maendeleo ya watu duniani yameshuka

Gerald Shiranda ni mwakilishi wa Uganda katika bunge la jumuiya ya afrika mashariki EALA

"Ukienda kugombania uongozi watu wanaangalia una fedha kiasi gani"

Mkutano huo umemalizika leo alasiri, makamishna wa Umoja wa Afrika wakiahidi kushirikiana na mahamaka ya haki ya Afrika kujitokeza na mkakati wa kushinikiza mataifa kuboresha huduma zaki kijamii na kiuchumi.