1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Wanaharakati waitisha maandamano makubwa Iran

5 Desemba 2022

Wanaharakati nchini Iran wameitisha wimbi jipya la maandamano ya umma kuanzia leo Jumatatu wakinuwia kusababisha hasara kubwa kwa uchumi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu inayoandamwa na vurugu kwa zaidi ya miezi miwili.

https://p.dw.com/p/4KTx5
Iran I Streik in Tehran
Picha: UGC

Chini ya wito huo mpya, wanaharakati hao wameomba raia wa Iran kutofanya manunuzi yoyote katika muda wa siku tatu zinazokuja ili kuzuia mzunguko wa fedha kwenye mfumo wa kibenki wa nchi hiyo.

Pia wamewarai wafanyabiashara kuyafunga wa maduka hususani kwenye miji mikubwa hadi siku ya Jumatano. Iran imekumbwa na wimbi la maandamano ya nchi nzima tangu kutokea kifo cha binti Mahsa Amini, aliyekamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kutofunika nywele zake vizuri.

Miito ya maandamano na migomo inajiri licha ya duru kadhaa za habari kusema mamlaka za Iran zimefikia uamuzi wa kukifuta kikosi cha polisi wa maadili kinachoshutumiwa kwa uonevu.