1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati nchini Ethiopia wakabiliwa na kifungo kwa shutuma za uchochezi

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfrj

ADDIS ABABA:

Mahakama moja nchini Ethiopia imewahukumu wana harakati wawili kwa uchochezi dhidi ya serikali.

Wanaharakati hao walikamatwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.

Watu hao wawili ndio wa mwisho kati ya 131 waliokamatwa na kushtakiwa baada ya ghasia zilizotokea kufuatia uchaguzi mkuu.

Uchunguzi wa bunge unasema kuwa watu 199 wakiwemo polisi waliuliwa na watu elf 30 kukamatwa wakati wa siku za ghasia baada ya wapinzani kudai kuwa kulikuwa na uibiaji wa kura.

Wakipatwa na hatia watakwenda jela miaka 10 na kesi yao inaamuliwa jumatano ya wiki hii.