1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanahabari wajadili 'migawanyiko' ya ulimwengu kwenye GMF

19 Juni 2023

'Kuishinda Migawanyiko' ndiyo maudhui ya mara hii kwenye Jukwaa la Vyombo vya Habari vya Ulimwengu lililoandaliwa na Deutsche Welle, likiwakusanya pamoja washiriki wapatao 2,000 kutoka pande mbalimbali za dunia.

https://p.dw.com/p/4SleZ
GMF 2023 | Opening Session | Peter Limbourg
Picha: Florian Goerner/DW

Kongamano hilo lililofanyika mjini Bonn siku ya Jumatatu (Juni 19) lilifunguliwa kwa kikundi cha waimbaji waliofunika nyuso zao kutoka nchini Belarus kuwatumbuiza washiriki kutoka mataifa ya Ulaya, Asia, Afrika na Amerika waliokuwa wanakutana kuiangalia nafasi ya vyombo vya habari kwenye kuipatanisha dunia iliyogawika. 

Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle, Peter Limbourg, aliiambia hadhara iliyokusanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano kwamba migawanyiko iliyopo duniani inahusu kila sekta na kila nyanja za maisha, na hivyo kuishinda ni wajibu wa awali wa kila mwanahabari anayeishi kwenye zama za sasa.

Sikiliza: 

"Tunapozingatia kuongezeka kwa migawanyiko ya kijamii katika maeneo mengi ulimwenguni, vyombo vya Habari vina wajibu maalum. Habari za uongo, nadharia potofu na siasa za hamasa ni changamoto kubwa inayoikabili tasnia yetu. Jukwaa hili la Vyombo vya Habari ndipo mahala pa kuufanikisha ushindi dhidi ya hayo, kwani hapa tunabadilishana mawazo na uzoefu." Alisema Limbourg.

Bobi Wine: Mataifa ya Magharibi hayakuleta demokrasia kwetu

Mbali na Limbourg, mwengine aliyezungumza kwenye ufunguzi wa kongamano hili ni Waziri wa mambo wa Kigeni wa Ujerumani, Analena Bearbock, ambaye aligusia jinsi vita vya Urusi nchini Ukraine vilivyoweka wazi hatari zilizopo pale migawanyiko isipopatiwa ufumbuzi haraka na pale watawala wanapoamua kuunyamazisha ukweli na kuupa sauti uongo. 

Ukosefu wa uadilifu kama chanzo cha migawanyiko

Hata hivyo, kongamano hilo limeambiwa kuwa migawanyiko inachangiwa pia na ukweli kuwa ulimwengu unaojiita wa kizio cha kaskazini unajimilikisha peke yake usahihi wa fikra na mawazo ya kuiendesha dunia, huku ule uitwao kizio cha kusini ukiwachwa nyuma. 

Akipigia mfano juu ya uendeshaji wa Umoja wa Mataifa – kama taasisi kuu ya kilimwengu – mwanaharakati wa haki za wanawake na mshindi wa Tuzo ya Nobel kutoka Liberia, Leymah Gbowee, alisema ukosefu huu wa uadilifu ni chanzo cha migawanyiko.

GMF 2023 | Rede NRW-Ministerpräsident Hendrik Wüst
Waziri Mkuu wa jimbo la Northrhine Wesphalia, Hendrik Wüst, akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la 16 la Global Media Forum.Picha: Florian Goerner/DW

Soma zaidi: Hakuna usawa wa habari baina ya mataifa tajiri na masikini - Washiriki

"Kwenye dunia tunayoishi leo, kuna haja ya kuondosha nafasi ya wajumbe watano wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Miaka 75 iliyopita wakati Umoja wa Mataifa unaanzishwa kulikuwa na ukoloni ambao haukuruhusu nchi zijisemee, leo hii tena kwa nini tuna chombo chenye wajumbe watano tu wa kudumu?" Alihoji mwanaharakati huyo.

Mshindi wa Tuzo ya Uhuru wa Habari


Kongamano la mara hii linafanyika kwa siku mbili na zaidi ya mataifa 120 yametuma wawakilishi wao kuhudhuria.

Chini ya mwamvuli wa maudhui ya 'kuishinda migawanyiko', mada kadhaa zimejadiliwa leo, ikiwemo ya matumizi salama ya majukwaa ya mitandao ya kijamii na jukumu la wanahabari kwenye maeneo yenye migogoro. 

Mbali na mikutano na mijadala, kongamano hili pia linapambwa kwa Tuzo ya Uhuru wa Habari ya DW ambayo mwaka huu ametunukiwa mwandishi wa Habari za uchunguzi kutoka nchini El Salvador, Oscar Martinez.

Edward Mutebi | GMF 2023 | Menschenrechtsaktivist
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Global Media Forum 2023 mjini Bonn.Picha: Konrad Hirsch