Ufaransa yapiga marufuku Abaya shuleni
2 Septemba 2023Rais Macro ameeleza kwamba mamlaka zitakuwa thabiti katika kutekeleza sheria hiyo mpya, masomo yatakapoanza tena wiki ijayo.
Wakati wa mkutano na wanahabari siku nne zilizopita, waziri wa elimu nchini humo Gabriel Attal alitangaza kuwa nguo zinazovaliwa hasa na waislamu zinazojulikana kama abaya kwa wasichana na wanawake na khamis kwa wavulana na wanaume, zitapigwa marufuku wakati wa kuanza kwa mwaka mpya wa shule siku ya Jumatatu.
Wanafunzi watakaovaa mavazi marefu watakiuka kanuni ya msingi ya Ufaransa
Macron alizungumzia kanuni hiyo ya mavazi kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kutembelea shule moja katika eneo la Vaucluse kusini mwa Ufaransa.
Macron amesema anajuwa kutakuwa na visa vya wanafunzi kuijaribu sheria hiyo pamoja na wale watakaojaribu kupinga mfumo huo.