1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanadiplomasia wa UN watoa mwito wa mshikamano duniani

4 Mei 2023

Wanadiplomasia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamependekeza njia zinazoweza kutumika kuielekeza dunia katika mustakhbali wa amani zaidi, wakisema ni kazi ngumu lakini inawezekana.

https://p.dw.com/p/4Qssm
Marekani, New York | Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Ukumbi wa mikutano ya Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: Ed Jones/AFP/Getty Images

Nchi zilizogawika zilikubaliana jana kwamba kuna ukosefu wa uaminifu katika dunia inayokabiliwa na machafuko na migogoro. Waziri wa mambo ya nje wa Uswisi Ignazio Cassis, alichagua mjadala kuhusu uaminifu, akiutaja kuwa kipengele muhimu cha amani.

Cassis pia alisema diplomasia ya kimataifa inakabiliwa na shinikizo na wanachama wa Umoja wa Mataifa sharti watambue hawajazingatia hali ya kukatisha tamaa na changamoto zinazoikabili dunia.

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia ameanisha changamoto iliyopo ya kujenga madaraja akigusia mpasuko uliopo na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa nchi 15 wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.