Wanachumi watakiwa wazidishe juhudi za kubuni nafasi za kazi Ujerumani
28 Machi 2005Matangazo
Berlin:
Kansela Gerhard Schröder amewataka wanauchumi wafanye zaidi kuinua ukuaji wa kiuchumi na kubuni nafasi zaidi za kazi nchini Ujerumani.Katika mahojiano na gazeti la "Bild am Sonntag" kansela Gerhard Schröder amesema mpango wa mageuzi ulioandaliwa na serikali yake, mashuhuri kwa jina "Ajenda 2010" unawarahisishia mambo wanauchumi.Kansela Gerhard Schröder amezungumzia juu ya hatua zaidi zilizopitishwa.Ameyatolea mwito mashirika ya viwanda yasitishe mitindo ya kuhamia ng’ambo na kuweka vitega uchumi zaidi nchini Ujerumani.Wanasiasa wa upande wa upinzani wanautaja mwito wa kansela kua ni "mbinu za kuwafumba watu midomo."