1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanachama wapya kukaribishwa NATO

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJia

BRUSSELS:

Mawaziri wa Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi-NATO wanakutana mjini Brussels kujadili upanuzi wa muungano huo kwa kupokea wanachama wapya watano.Miongoni mwa mataifa yanayozingatiwa ni Ukraine na Georgia-majimbo yaliyokuwa sehemu ya Soviet Union ya zamani.Wadadisi wa kisiasa wanasema,hatua za kuzingatia uanachama wa mataifa hayo mawili,huenda zikazidisha mvutano kati ya Nato na Moscow.

Mkutano wa Brussels pia utajaribu kupunguza mvutano uliozuka kufuatia ombi la Macedonia kutaka kuwa mwanachama.Ugiriki imetishia kupinga ombi hilo kwa sababu ya ugomvi wa miaka mingi kati ya nchi hizo mbili unaohusika na jina la Macedonia.