1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanachama wa SPD waidhinisha ilani ya uchaguzi

Sekione Kitojo
26 Juni 2017

Chama cha Social Democratic Ujerumani kimemuunga mkono kiongozi wake Jumapili,(25.06.2017)kikikubali sera za uwekezaji,haki za kijamii na Ulaya na kinamatumaini hatua hizo zitabadilisha upunguaji wa mvuto wa wapiga kura 

https://p.dw.com/p/2fNlr
Deutschland SPD-Bundesparteitag
Picha: Reuters/W. Rattay

Chama hicho kinakinataka  kuungwa  mkono  na wapiga kura  na kuifikisha mwisho  safari ya  kansela Angela  Merkel kuwapo  madarakani  kwa muda  wa  miaka  12  katika  uchaguzi  utakaofanyika  mwezi Septemba.

Katika  mkutano  uliokuwa  na  msisimko  mkubwa , kiongozi wa  SPD Martin Schulz  amemshutumu  kansela  wa  Ujerumani  Angela Merkel  kwa  kuzima  mjadala  kuhusiana  na  masuala  kama  mafao ya  uzeeni  na  kushindwa  kusimama  imara  dhidi  ya  Marekani.

Deutschland SPD-Parteitag in Dortmund
Mgombea wa chama cha SPD Martin Schulz Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Chama  cha  SPD kimepata  nguvu  kubwa  katika  maoni  ya wapiga  kura  baada  ya  Schulz  kutangazwa  kuwa  kiongozi  wa chama  hicho  mwezi  Januari mwaka  huu, akikipita   chama  cha kansela  Merkel  cha  CDU, katika  baadhi ya  mambo,  lakini mafanikio  hayo  yameyeyuka  hivi  sasa  na  chama  kinahangaika kurejea  katika  njia  yake. Kansela  wa  zamani Gerhard Schroeder amehamasisha  katika  mkutano  huo kwa  kusema  inawezekana kubadilisha  hali  hiyo.

"Iwapo tutakusanya nguvu  zetu  zote  katika  wiki  chache  zijazo  na kupambana kutafuta  kila  kura, tunaweza  kufanikiwa  kukifanya chama  cha  SPD kuwa  chama  kikubwa."

Katika  hotuba iliyochukua  dakika  80  kabla  ya  chama  hicho kukubaliana  na  sera zilizomo  katika  ilani ya uchaguzi, Schulz  rais wa  zamani  wa  bunge  la  Ulaya, alionesha  mapenzi  makubwa  kwa Umoja  wa  Ulaya.

Deutschland | SPD rüstet sich für den Parteitag
mabango katika mkutano mkuu wa chama cha SPD uliomalizika Jumapili 25.06.2017 mjini DortmundPicha: Reuters/W. Rattay

Kiburi cha  madaraka

Merkel  na  waziri wa  fedha Schauble  wako  imara  sana zinapokuja  sera  kama  kubana  matumizi kwa mataifa ya Ulaya lakini  husikii  chochote kutoka  kwao  juu  ya  utawala  wa  sheria na demokrasia katika  Umoja  wa  Ulaya,  ameyasema  haya  akiilenga Hungary na  Poland.

Amesema  chama  cha  SPD kinalenga  kuimarisha Ulaya  na kusisitiza  maadili  ya  utu na  kuwekeza  katika kuweka  hali  mpya.

Nafasi  ya  kumnyima  Merkel muhula wa nne inaonekana  kuwa finyu kwa  SPD, chama  ambacho  ni mshirika mdogo  katika  serikali  ya muungano  wa  siasa  za  wastani  za  mrengo  wa  kulia  na kushoto, lakini baadhi wametiwa moyo  na  kile  kilichotokea Uingereza  ambapo chama  cha  Labour chini  ya  Jeremy Corbyn kilibadilisha  mambo  katika  uchaguzi  wa  hapo  Juni 8.

Deutschland  Saar-SPD stimmt über Koalitonsvertrag ab
Wanachama wa SPD wakipiga kura kuidhinisha ilani ya uchaguziPicha: picture alliance/dpa/O. Dietze

Martin Shulz alimshambulia  kansela  Merkel kwa  kumshutumu  kuwa na  kiburi  katika  mambo  kadhaa  ya  uongozi.

Wakati chama kinasema  hatuna  chochote  cha  kufanya  kuhusu hili na  hatuwezi  kujadili  hili katika  kipindi  cha  kampeni, hii  ni kiburi cha madaraka, hakuna  kingine, wapenzi mabibi  na  mabwana."

Kukiwa  kumebakia  wiki  kadhaa  kabla  ya  Ujerumani  kuingia katika  uchaguzi  hapo  Septemba  24 , chama  cha  SPD  kiko nyuma  ya  chama  cha  kansela Angela  Merkel  cha  Christian Democratic Union CDU  kwa  asilimia  15  ya  alama, kwa  mujibu wa  uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura  uliochapishwa jana Jumapili  na  gazeti  la Bild.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Josephat Charo