1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamiliki wa Blogi Tanzania wapewa muda wa mwisho kujisajili

Sekione Kitojo
24 Aprili 2018

Mamlaka  ya  Mawasiliano nchini  Tanzania  imetoa  muda wa  mwisho  wa  wiki  mbili  kwa  wamiliki wa blogu kuandikisha  mitandao yao  chini  ya  sheria  kali  za maudhui  ya  mitandao  ya  kijamii.

https://p.dw.com/p/2wYzQ
YouTube Gewalt Symbolbild
Picha: picture-alliance/dpa/N. Armer

Mamlaka  ya  Mawasiliano nchini  Tanzania  imetoa  muda wa  mwisho  wa  wiki  mbili  kwa  wamiliki wa blogu kuandikisha  mitandao yao  chini  ya  sheria  kali  za maudhui  ya  mitandao  ya  kijamii, huku  kukiwa  na  wasi wasi  kwamba  serikali inabana  uhuru  wa  watumiaji  wa mtandao  wa  intaneti.

Sheria  iliyopitishwa  mwezi  Machi  inafanya  kuwa  lazima kwa  wenye  blogu  na  wamiliki  wa  majukwaa  ya mtandaoni  kama   televisheni  za  mtandao  wa  Youtube kujiandikisha  katika  serikali  na  kulipa  kiasi  cha  dola 900 sawa  na  zaidi  ya  shilingi  za  Tanzania  milioni 2  ili kupata  leseni. 

Wanaharakati  wa  kidijitali  wanasema  hatua  hiyo  ni sehemu nyengine ya ukandamizaji  wa  serikali  dhidi  ya upinzani  na  uhuru  wa  kutoa  maoni  unaofanywa  na serikali  ya  Rais  John Pombe  Magufuli, ambaye alichaguliwa  mwaka  2015 na  kuahidi  kuharakisha  ukuaji wa  uchumi  na  maendeleo.

Waombaji  wanatakiwa  kutoa  maelezo  ya  wadau, mtaji, uraia  wa  mmiliki, ujuzi wa  wafanyakazi na  mipango  ya mafunzo, pamoja  na  hati  ya malipo  ya  kodi.