1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliopigania ukombozi wakamatwa Zimbabwe

28 Julai 2016

Mhemko wa kisiasa unazidi kushuhudiwa kiongozi wa chama cha waliopigania ukombozi wa taifa hilo amekamatwa baada yakundi hilo kumtuhumu rais Robert Mugabe kuwa dikteta

https://p.dw.com/p/1JXQj
Rais Robert Mugabe akihutubia wafuasi wake 27 julai 2016 Harare
Rais Robert Mugabe akihutubia wafuasi wake 27 julai 2016 Harareobert MugabePicha: picture alliance/dpa/A. Ufumeli

Jumatano rais Robert Mugabe alitoa onyo kali dhidi ya wakongwe wa vita vya ukombozi waliotoa kauli ya kumponda rais huyo wiki iliyopita na akaapa kuchukua hatua kali dhidi yao.

''Tumeanzisha timu ya uchunguzi ndani ya chama kubaini waliohusika kuandika taarifa hiyo.Tunataka kufahamu kina nani waliohusika na kuichapisha.Tukiwapata wahusika wataadhibiwa ipasavyo.Na adhabu hiyo itakuwa adhabu kali kabisa''

Waliopigania ukombozi katika vita vya uhuru miaka ya 1970 ambao awali walikuwa ni wafuasi watiifu wa rais Mugabe walitoa taarifa inayomkosoa na kumuumbua kikamilifu rais huyo mwenye umri wa miaka 92 ambaye anaendelea kukabiliwa na ishara za kupingwa ndani ya chama chake.Douglas Mahiya msemaji wa kundi hilo la waliopigania ukombozi wa Zimbabwe akizungumza kwa jazba alimkosoa Mugabe akisema hapaswi kuendelea kuwemo ndani ya chama cha Zanu PF.

Maelfu ya wafuasi wa chama cha Zanu Pf waliomiminika katika mkutano Harare
Maelfu ya wafuasi wa chama cha Zanu Pf waliomiminika katika mkutano HararePicha: picture alliance/dpa/A. Ufumeli

Kwanini hatuheshimiwi.Chuki tunayofanyiwa na watu walioko madarakani kutokana na kujitolea kwetu muhanga ni ile ile tuliyokuwa tukifanyiwa na Smith.hakuna tafauti.wanataka twende wapi.hatuendi mahala kokote.Sisi ndio msingi wa chama hiki.Anayeshindwa kutuelewa sisi katika mtazamo wa kimapinduzi anapaswa kuondoka yeye.

Douglas Mahiya lakini baada ya kauli hiyo alikamatwa jana jioni mjini Harare kwa mujibu wa kundi la wanasheria wa kutetea haki za bindamu ZLHR: Hadi kufikia sasa taarifa zinazofahamika zinasema kwamba polisi wanamshtaki mwanaharakati huyo wa vita vya ukombozi kwa kosa la kuihujumu serikali iliyoko madarakani kwa mujibu wa katiba pamoja na kuidhalilisha ofisi ya rais.Aidha wakili wa familia ya Mahiya amethibitisha juu ya kukamatwa kwa mpiganaji huyo wa zamani.

Kadhalika ripoti zimeeleza kwamba katibu mkuu wa chama hicho cha wapiganaji wa zamani wa vita vya ukombozi Victor Matemandanda alichukuliwa kutoka nyumbani kwake kijijini huko Gokwe kaskazini magharibi mwa Zimbabwe baada ya kuhojiwa na polisi.Hdai kufikia wakati huu hajulikani aliko kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini Zimbabwe. Kundi hilo la waliopigania ukombozi wiki iliyopita lilitoa msimamo wake na kuapa kutomuunga mkono Mugabe ambaye amekuwepo madarakani tangu mwaka 1980 ikiwa ataamua kugombea tena urais mwaka 2018.

Moja ya maandamano mjini Bulawayo
Moja ya maandamano mjini BulawayoPicha: Getty Images/AFP/Stringer

Wachambuzi wa mambo nchini Zimbabwe wanasema unyamazishaji wapinzani na wakosoaji unaweza ukaendelea kushuhudiwa lakini hasira za wananchi haziwezi kuzuilika.

Mwandishi :Saumu Mwasimba

Mhariri:Josephat Charo