Waliokufa kwenye miripuko ya Nigeria wafikia 160
22 Januari 2012Jana (21.01.2012), mji wa kaskazini wa Kano ulikuwa hauna watu , baada ya kuwekwa amri ya kutotoka nje. Mashambulizi hayo yalilenga kiasi cha maeneo sita katika mji huo ikiwa ni pamoja na ofisi za polisi na uhamiaji pamoja na eneo la kuegesha magari jioni ya Ijumaa.
Serikali ya Nigeria inawatuhumu wanamgambo wa kundi la Boko Haram kuhusika na mashambulizi hayo. Mwezi uliopita, mtu anayesemekana kuwa msemaji wa kundi hilo, alisema kwamba kundi lake lilihusika na mashambulizi ya mabomu katika siku ya Krismasi, ambayo yalielekezwa dhidi ya makanisa. Agosti mwaka jana, jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja lilishambuliwa pia kwa mabomu, na tena kundi la Boko Haram likatajwa kuhusika.
Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef