Waliokufa kwa kuacha kula Kenya wapindukia watu 300
14 Juni 2023Matangazo
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha alisema idadi ya waliofariki hadi wakati huu imeongezeka na kufikia watu 303 baada ya miili 19 kufukuliwa.
Polisi ya inaamini kuwa miili mingi iliyopatikana katika msitu karibu na mji wa Malindi katika Bahari ya Hindi ni ya wafuasi wa Paul Nthenge Mackenzie, dereva wa teksi ambaye amegeuka kuwa mhubiri ambaye amekuwa chini ya ulinzi wa polisi tangu Aprili 14.
Soma pia: Kenya kuugeuza msitu wa Shakahola kuwa kituo cha kumbukumbu
Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kukabiliwa na mashtaka ya "ugaidi" katika kesi ambayo imetikisa taifa hilo la Afrika mashariki.