1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIndonesia

Idadi ya waliokufa tetemeko Indonesia yafikia 268

22 Novemba 2022

Rais wa Indonesia Joko Widodo ameahidi kuwa miili ya watu ambayo haijaonekana bado kufuatia tetemeko la ardhi itapatikana baada ya kutembelea eneo lililoathirika katika wilaya ya Cianjur.

https://p.dw.com/p/4JuKu
Indonesien | Erdbeben in West-Java | Rettungskräfte
Picha: Aditya Irawan/NurPhoto/IMAGO

Tetemeko hilo lililoukumba mkoa wa Java Magharibi limeuwa watu wasiopungua 268 mpaka sasa, wengi wao wakiwa watoto, na maafisa wa uokozi wanasema watu wengine 151 bado hawajulikani walipo.

Tetemeko hilo la ukumbwa wa 5.6 liliupiga mkoa wa Indonsia wenye idadi kubwa zaidi ya watu Jumatatu mchana, na kusababisha uharibifu mkubwa katika mji wa Cianjur, ulioko umbali wa takribani kilomita 75 kusini-magharibi mwa mji mkuu Jakarta, na kukifunika alau kijiji kimoja chini ya maporomoko ya udongo.

Mkuu wa shirila la kushughulikia majanga Suharyanto, amewambia waandishi habari kuwa zaidi ya watu 1,000 wamejeruhiwa, elfu 58 wamepoteza makaazi na nyumba elfu 22 zimeharibiwa.

Indonesien | Erdbeben in West-Java | Rettungskräfte
Muokoaji akitembea katika vifusi vya jengo lililoharibiwa wakati wa operesheni ya uokozi baada ya tetemeko mjini Cianjur, Java Mashariki, Indonesia, Novemba 22, 2022.Picha: Yulius Satria Wijaya/Antara Foto/REUTERS

Naye mkuu wa shirika la taifa la utafutaji wa uokozi, Henri Alfiandi, amesema maporomoko ya udongo na hali mbaya vilitatiza juhudi za uokoaji.

Soma pia: Waliokufa kwa tetemeko la ardhi Indonesia wapindukia 260

Rais Joko Widodo amesafiri kwenda mjini Cianjur Jumanne kuwapa moyo waokoaji, na kuwagiza kutoa kipaumbele kwa utafujaji wa watu wanaoendelea kukwama chini ya vifusi.

"Tayari nimeagiza wahanga waliofunika bado kuondolewa na kushughulikiwa kwa kipaumbele na mara moja," alisema Widodo baada ya kuzuru eneo la tukio.

Tetemeko dogo, athati kubwa

Wakati mateteko makubwa ya kiwango cha 6 au 7 yamezoelekwa kwa kiasi nchini Indonesia, wataalmu wanasema tetemeko la Jumatatu ambalo kiwango chake ni kidogo lilikuwa ana madhara makubwa kwa sabab lilipiga kwenye ardhi kwenye kina kifupi.

Maafisa wanasema watu wengi wameuawa kufuatia kuporomoka kwa majumba yaliojengwa vibaya, huku rais aikitoa wito kwa juhudi za ujenzi mpya kuhusisha vidhibiti vya matetemeko ya ardhi. 

Indonesien | Erdbeben in West-Java | Rettungskräfte
Waokoaji wakiutoa mwili wa muhanga wa maporomoko ya udongo yaliosababishwa na tetemeko la ardhi mjini Cianjur, Java Magharibi, Indonesia, Jumanne, Novema, 22, 2022.Picha: Rangga Firmansyah/AP Photo/picture alliance

Maafisa wanaoshughulikia majanga wamesema wataelekeza juhudi kwenye moja ya maeneo yalioathiriwa vibaya zaidi ya Cugenang, ambalo lilikumba na mporomoko wa udongo uliosababishwa na tetemeko hilo.

Vituo vya habari vya televisheni vimeonyesha picha za watu walichimba udongo wa kwa kutumia jembe, nondo na zana nyingine.

Mkuu wa polisi ya taifa Listyo Sigit Probowo, amesema zaidi ya askari polisi 1,000 wamepelekwa kusaidia shughuli ya utafutaji.

Soma pia: Watu 920 wafa kwa tetemko la ardhi Afghanistan

Ikiwa juu ya kile kinachojulikana kama mduara wa moto, ambao ni ukanda hai wa matetemeko ambako mabamba tofauti ya tabaka la juu la dunia hukutana, Indonesia imekuwa na historia ya kukumbwa na mateteko mabaya.

Mnamo mwaka 2004, tetemeko lenye ukubwa wa 9.1 nje ya kisiwa cha Sumatra kaskazini mwa Indonesia lilisababisha sunami iliyoyatikisa mataifa 14, na kuuwa watu 226,000.

Chanzo: mashirika