1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Walinzi watatu wa amani wa Umoja wa Mataifa wauwawa Mali

22 Februari 2023

Wanajeshi watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa baada ya kutokea mripuko wa bomu lililotegwa barabarani katikati mwa Mali.

https://p.dw.com/p/4Np5K
Symbolbild I MINUSMA in Mali
Picha: Sia Kambou/AFP

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema mripuko huo ulitokea karibu na kijiji cha Songobia, wakati askari hao wakitawanywa katika utaratibu wao wa kazi chini ya kikosi cha pamoja cha kulinda amani nchini humo kijulikanacho kama MINUSMA.

Kupitia taarifa tofauti, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres, wameyalaani vikali mashambulizi hayo, waliyosema yanaweza kuwa uhalifu wa kivita kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa.

Baraza hilo la usalama limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama nchini Mali na mwelekeo wa kimataifa wa kitisho cha ugaidi katika eneo la Sahel.

Limesema amani katika ukanda huo haitapatikana bila ya kuwepo mchanganyiko wa juhudi za kisiasa, kiusalama, ujenzi wa amani na maendeleo ambazo kwa pamoja zitasaidia mikoa yote ya Mali na utekelezaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2015.