1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUswisi

Mkutano wa WEF wamalizika. Lipi limefikiwa huko?

19 Januari 2024

Viongozi wa kibiashara na kisiasa wamesema wanageukia mazingira yatakayoimarisha ugavi wa bidhaa muhimu na kupunguza athari zinazowezakana kutokana na migogoro isiyotarajiwa ya kisiasa na kijiografia.

https://p.dw.com/p/4bTUD
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani, WEF 2024 | Davos
Jukwaa la Kimataifa la Uchumi, WEF limemalizika katika mji wa Davos Januari 19, 2024 likitoa wito wa kutatuliwa mizozo ulimwenguniPicha: Lian Yi/Xinhua News Agency/picture alliance

Jukwaa la Kiuchumi Duniani, WEF limemalizika Ijumaa huko mjini Davos, Uswisi.

Jukwaa hilo mwaka huu limefanyika huku likitawaliwa na mizozo ya Mashariki ya Kati na Ukraine, pamoja na uchaguzi unaokaribia kwenye nchi kadhaa.

David Garfield, afisa anayeshughulikia masuala ya viwanda kwenye taasisi mashuhuri ya maendeleo ya Alix Partners,  amesema wakati tu serikali na makampuni yanapopata njia ya kukabiliana na mlipuko mmoja, mwingine unaibuka.

Garfield amesema kampuni za kisasa zinajiuliza zifanye nini iwapo malighafi ya uzalishaji muhimu utapunguzwa.

Wajumbe wengi wameelezea jinsi hali ya ulimwengu ilivyo ya kuhuzunisha isivyo ya kawaida.