1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa majeshi mataifa 22 kuijadili IS

14 Oktoba 2014

Makamanda wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislamu wanakutana Washington leo hii kwa lengo la kujadili namna ya kudhibiti kusonga mbele kwa wapiganaji wa kundi hilo.

https://p.dw.com/p/1DVJo
Kämpfe um Kobane 13.10.2014
Mapigano mjini KobanePicha: Reuters/Umit Bektas

Hayo yanakuja wakati ambapo ya anga yakishindwa kuwadhibiti wanamgambo kufika katikati ya Kobane.

Hadi jana kundi la Dola ya Kiislamu lilionekana kudhibiti karibu nusu ya mji huo tete, uliopo katika eneo ma mpaka wa Syria na Uturuki pamoja na kuwepo kwa mashambulizi ya kutokea angani yenye lengo la kuzuia jitihada zao, yanayoongozwa na Marekani kwa takribani wiki tatu. Huyu ni mmoja kati ya watu wa jamii ya Kikurd

Kushindwa kwa operesheni hiyo kutakuwa miongoni mwa ajenda muhimu katika mkutano huu wa Washington wa wakuu wa majeshi kutoka matiafa 22, katika muungano unaoongozwa na Marekani. Inategewema pia katika mkutano huo kwamba Uturuki itatoa wito wa kuwekwa kanda huru isiyo ya mapigano itakayolindwa katika eneo lake na mpaka wa Syria.

Barack Obama
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: Reuters/G. Cameron

Mkutano wa makamanda na Obama

Nayo Ikulu ya Marekani imesema maafisa wa ngazi ya juu, wakiwemo wakuu wa majeshi vilevile watakutana na rais Barack Obama katika kambi ya jeshi la anga ya Andrews, nje kidogo ya jiji la Washington.

Msemaji wa mwenyekiti wa muungano wa wakuu hao wa majeshi, kanali wa Kimarekani, Ed Thomas amesema, majenerali hao watajadili juu ya kuwepo kwa msimamo wa pamoja wa kukabilina na Dola ya Kiislamu, changamoto na mikakati mingene ya baadae.

Mataifa yanayowakilishwa katika mkutano huo ni Australia, Bahrain, Ubeligiji, Uingereza, Canada, Denmark, Misri, Ufaransa, Ujerumani, Iraq, Italia, Jordan, Kuwait, Lebanon, Uholanzi, New Zealand, Qatar, Saudi Arabia, Uhispania, Uturuki, Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Marekani kama taifa mwenyeji.

Hii natajwa kuwa ni mara ya kwanza kabisa kufanyika kwa mkutano kama huo unaohusisha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi, tangu tangu mataifa hayo yajiunge pamoja Septemba. Miongoni mwa fikra zinazotolewa katika mkutano huo ni hilo la kuwepo kwa ukanda huru usio wa mapigano, katika eneo la mpaka la Uturuki na Syria, ambalo wanachama wa muungano huo wanapingana nalo na Marekani ikisema lisigubike ajenda.

Na katika mashambulizi ya hivi karibuni, ndege za kivita za Marekani na Saudi Arabia zimelenga maeneo saba mjini Kobane, ambapo jeshi la Marekani linasema , yamo ambayo yalikuwa yakitumiwa na Kindo la Dola la Kiislamu kuingia katikati ya mji huo.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman