Mahakama Kuu nchini Tanzania kanda ya Dar es Salaam imesema sheria ya uchaguzi inayowapa uhalali wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ni batili, na hivyo imetamka kuvifuta vipengele viwili katika sheria hiyo. Mahakama hiyo imesema, imejiridhisha pasi na shaka kuwa wakurugenzi hao hawapaswi kuwa sehemu ya usimamizi wa uchaguzi kwa vile hawako huru.