Wakongo kuhamishwa kuruhusu uchimbaji wa madini ya dhahabu
23 Julai 2010Matangazo
Watu 15 elfu watahamishwa makwao ili kurahisisha uchimbaji wa madini ya dhahabu na kampuni ya Uingereza na Afrika ya Kusini ya ANGLOGOLD kwenye vijiji kadhaa vya vimbo la Orientale, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kampuni hiyo imeahidi kuwajengea makaazi mapya na kuunda ajira. Mradi huo umezusha tofauti kubwa baina ya serikali na mashirika ya kiraia ya jimbo hilo ambayo yamehisi kwamba hatua ya kuhamishwa kwa raia bila hiari yao inakiuka haki za binadamu, huku wanaharakati wa kimazingira wakionyesha pia wasiwasi wao kuhusu hatua hiyo ya serikali na kampuni ya Anglogold. Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo
Mwandishi:Saleh Mwanamilongo
Mhariri:Josephat Charo