Upatikanaji wa chakula ni moja ya masuala ya msingi kwa mkimbizi yeyote duniani, pamoja na usalama, matibabu na mahala pa kulala. Kwa muda mrefu wakimbizi wamekuwa wakipewa chakula lakini sasa shirika la chakula duniani WFP limeanzisha mfumo wa kuwapa wakimbizi pesa taslimu. Katika makala yake, Emmanuel Lubega anaangazia faida na changamoto za mfumo huo.