Matangazo
Uamuzi huo unafuatia madai ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kwamba Kenya inawalazimisha wakimbizi wa kisomali kurejea kwao katika jitihada za kuifunga kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Dadaab. Kenya inasema Wasomali wanarejea nchini kwao kwa hiari. Katika Kinagaubaga, Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Josephat Charo, amezungumza na Mkurugenzi wa Shirika la wakimbizi la Danish Refugee Council, tawi la Kenya.