Kwa mara nyingine DW inakukaribisha katika makala inayokupasha habari juu ya matukio na masuala ya barani Ulaya. Haya ni makala ya Mwanagaza wa Ulaya na wiki hii tunaangazia hali inayowakabili wahamiaji kutoka Afrika walioko nchini Italia, kukiwa na taarifa kwamba watu hao waliozikimbia nchi zao wanafanyishwa kazi kwenye mashamba kama watumwa.