17 Julai 2024
Matangazo
Wimbi la mabadiliko linazidi kupepea nchini Kenya na linabadilisha mawazo ya Wakenya wengi kugeukia dawa za kiasili na kuacha dawa za hospitalini. Wanaobadilishwa mawazo wanadai kuwa dawa za asili hazina madhara yoyote zikilinganishwa na dawa za hospitalini. Katika Makala ya Wanawake na Maendeleo leo Shisia Wasilwa anamwangazia mama Abigael Chebet anayeuza dawa za kiasili katika jimbo la Baringo nchini Kenya.