Uchumi
Wakenya waonywa kutobadilisha fedha kutumia mitandao haramu
22 Oktoba 2018Matangazo
Wakala wa masoko ya fedha nchini Kenya -CMA- umewaonya wakenya leo dhidi ya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kupitia mitandao isiyo na leseni. Wakala huo umeonya kwamba kuna hatari ya kupoteza uwekezaji wa fedha zao.
Mkurugenzi mtendaji wa wakala huo Paul Muthaura amesema amegundua watu kadhaa na mitandao mbali mbali wanafanya biashara hiyo ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mitandao ambayo hayajapewa leseni na vyombo vinavyohusika.
Ameongeza kuwa wakala huo wa masoko ya fedha za kigeni unapanga kuchukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wanaofanya biashara hiyo kinyume cha sheria.