Wakenya bado wasubiri uamuzi wa mahakama ya juu kabisa nchini humo
22 Machi 2013Matangazo
Katika kipindi hiki cha mpito nchini Kenya,ambapo wakenya wanasubiri mahakama kuu kutoa uamuzi wake juu ya kesi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais,asasi mbali mbali za kisheria na kikatiba zina kibarua cha kufafanua yaliyomo kwenye katiba mpya ili kuepuka mizozo na mkanganyiko katika hatua ya ukabidhi wa madaraka. Caro Robi alizungumza na mwenyekiti wa Tume ya utekelezaji katiba nchini Kenya Charles Nyachae kuhusu wajibu wa tume hiyo na ufafanuzi wa kuendeshwa kwa majukumu ya serikali kwa sasa. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Caro Robi
Mhariri:Yusuf Saumu