Wake wa viongozi Afrika himizeni ajenda ya uzazi wa mpango
9 Oktoba 2023Amesema hayo Angeline Ndayishimiye mke wa rais wa Burundi kwenye kongamano la 4 la wanawake viongozi lilizinduliwa Bujumbura.
Kongamano hilo la limehuudhuriwa na wake wa marais wa Kenya, Rwanda, Zanzibar na wale kutoka matawi mbali mbali ya Umoja wa Mataifa.
Wanawake viongozi wanalo jukumu la kuhakikisha uzazi wa mpango katika jamii, njia itakayoruhusu lishe bora na kufikia maendeleo endelevu, ni kauli mbiu hiyo inayojadiliwa katika mkutano huo ulozinduliwa hapa Bujumbura.
Soma pia:Mpango wa uzazi kwa njia ya homoni huongeza hatari ya saratani ya matiti
Mkutano huo uloandaliwa na kituo OPDD kinachoongozwa na mke wa rais, Bi amesema dhamira ya mkutano huo ni kukabiliana na ongzeko la watu kwani limekuwa likiathiri maenddeleo yanayokusudiwa.
"Tunatakiwa kuepuka uzazi pasina mpango, kwani hupelekea afya ya mwanamke kuzorota,"
Ameongeza kuwa watoto hulelewa bila uangalizi unaohitajika kwa makuzi ya watoto, huku mama akishindwa kujihusisha na shughuli za maendeleo ya jamii na hata ya nchi.
Mwanamke anabeba mtoto mmoja mgongoni, mwingine kwenye mapaja,
na mwingine akiwa tumboni. Magonjwa ya utapiamlo, kipato kinakuwa hafifu, ugomvi katika familia, huku migogoro ya ardhi ikifuatia. Alisema mke wa rais Angeline Ndayishimiye.
Uzazi wa mpango unalinda afya ya jamii
Kwa upande wake Bi Mariam Mwinyi, mke wa rais wa Zanzibar, amesema uzazi wa mpango unasaidia pia kupunguza vifo vya uzazi kwa zaidi ya asilimia
30.
Na kwamba Tanzaniabara kuna asilimia 81 ya wanawake wanaojifungua katika vituo vya afya na asilimia 86 kwa Zanzibar.
Soma pia:Utumiaji holela wa vidonge vya uzazi vya P2 kwa wasichana na hatari inayowakabili
Swala la uzazi wa mpango na lishe bora lazima liorodheshwe katika miradi mikuu ya serikali, kwa kubuni sera na mikakati inayofaa.
Alisema Abdoul Dieng, mwakilishi mkaazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Burundi.
Mkutano huo wafuatia mwingine wa aina hii ulofanyika mwenye Oktoba mwaka jana ambapo wanawake viongoziwalitakiwa kuzidisha juhidi ili kuboresha afya na licha ya mama na mtoto na vijana baleghe.