1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakazi wa msitu wa Mau, Kenya waondolewa

1 Novemba 2019

Serikali ya Kenya imeanza kuwatimua watu wanaoishi katika msitu wa Mau kwa njia haramu. Hata hivyo viongozi wa eneo la bonde la Ufa uliko msitu huo wanaomba muda zaidi.

https://p.dw.com/p/3SKio
Kenia Präsidentschaftswahl Wahlsieger Uhuru Kenyatta
Picha: Reuters/T. Mukoya

Lakini serikali ikishikilia kuwa haitafanya hivyo na badala yake itaanza kupanda miche milioni 10 kwenye msitu huo ambao ni chanzo hicho kikuu cha maji nchini humo baada ya kuondoka kwa waliouvamia.

Ilani ya ya siku 60 yakuondoka kwenye msitu huo ilikamilika jana, huku serikali ikishikilia kuwa asilimia 70 ya watu waliokuwa wameuvamia msituo huo wameshaondoka kwa hiari. Kamishna wa Mkuu wa Bonde la Ufa George Natembeya amesema kuwa watu 2200 wameshaondoka kwenye msitu huo wenye ekari 17000 na wengine 1100 wateteketeze makazi yao. Christine Cheruyot amekuwa akiishi kwenye msitu huo kwa muda wa miaka 20. Hajui anakokwenda na anajiandaa kuanza safari ya kuondoka kufuatia kumalizika kwa siku walizokuwa wamepewa ili wahame. "Kama Mungu amesema tutoke tutatoka na kama Mungu amesema turudi tutarudi, Mungu anaamua yote.” alisema Christine. 

Bolivien -  Nationalpark Madidi
Sehemu ya msitu ambako wakazi hao wanatakiwa waondoke.Picha: Imago/Hecke

Weldon Kirui kama tu Christine hajafahamu makazi mengine mbali na haya kwa zaidi ya miaka 30. Naye amevikusanya vitu vyote kuanza ukurasa mpya wa maisha. Ukurasa uliojaa kiza.

Mwezi Agosti mwaka huu, serikali ilitoa ilani kwa familia 10000 zinazoishi hapa tangu miaka ya tisini kuhama. Awamu ya pili ya kuhamisha familia hizo inaanza leo. Serikali imepokea baadhi ya haki miliki za ardhi pamoja na nyaraka nyingine kwa waliohama kwa hiari. Natembeya pia amewaonya watakaopinga uhamisho huo. Alisema "Kuna wengine wanaokaa ndani ya msitu wa mau,lakini pia kuna wanafunzi katika msitu wa Mau hao pia tumesema kufikia mwisho wa siku watoto watakuwa wamefunga mashule."

Lakini kilomita kadhaa kutoka Mau viongozi wa siasa wa bonde la ufa walikuwa wanaungana na wenzao kuiomba serikali kuongeza muda wa kuhama wamekosoa uwamuzi wa mahakama uliotupilia mbali kesi iliyowasilishwa na mawakili 35 na makundi ya kutetea haki za binadamu ya kusitisha kuondolewa huko. Johana Ng'eno ni mbunge. "Tungependa kuambia rais ya kwamba hao ni watu wako na ni Wakenya, watoto hawakufanya mitihani, watoto hawakuenda shule." alisema Ng'endo.

Awamu hii ya pili itakapokamilika serikali inapanga kuanza kuchunguza na kurekebisha mipaka kwenye awamu ya tatu kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vyote vya maji katika msitu wa Mau.